Hii ndio shule ya Uswidi/Sweden.

Kuanzia ule muda mtoto wako anapofikisha umri wa mwaka mmoja (1) anaweza kuanza shule ya mapema ya umma/chekechea. Hiyo shule ya mapema ya umma ni ya hiari. Kutoka majira ya vuli ya mwaka ambayo mtoto wako anafikisha miaka mitatu (3) basi mtoto anayo haki ya kwenda kwenye shule ya mapema ya umma/chekechea. Shule ya mapema ya Umma inajumuisha yaani inahusu masaa 15 kwa kila wiki pamoja na kwamba ni bila ada/malipo.

Kuanzia umri wa miaka sita (6) mwanafunzi anaanza darasa la shule ya mapema/chekechea. Baada ya hilo darasa la shule ya mapema, mtoto anaweza kuanza katika shule ya msingi au sambamba na muundo wa shule kama hizo. Kwa ajili ya watoto walio na umri wa miaka kati ya 6 hadi miaka 13 ipo nyumba ya burudani/kucheza-cheza/fritidshem ambayo inakuwa wazi kabla na baada ya masaa ya shule pamoja na wakati wa shule zinaporuhusiwa kwa mapumzika mafupi yanapojitokeza na hivyo watoto wanakaribishwa kufanya shughuli mbali mbali zenye manufaa tafauti. Ada hupangwa kufuatana na kipato/mshahara wa walezi wa watoto.

Nchini Sweden kuna ulazima kwa watoto wote kusoma, hiyo inamaanisha kwamba kwa mujibu wa sheria hiyo ndiyo sheria isemayo kila mwanafunzi anapaswa kwenda shule na kusoma kuanzia darasa la shule ya mapema hadi darasa la 9. Kama mwanafunzi ni mgonjwa lazima ripoti itolewe shuleni kwa kila siku ambayo mwanafunzi anakuwa nyumbani. Ni walezi wa mwanafunzi tu ambao ndio wanaopaswa kutoa hiyo ripoti ihusuyo kutohudhuria shule tokana na kuugua. Ripoti nyingine endapo itatolewa sio halali.

Huu utamaduni wa shule za Uswidi unaweza kutofautiana na uzoefu wako wa awali wa shule. Hii inaweza kumaanisha kuwa mahitaji mengine yamewekwa na matarajio kwa wote yaani wanafunzi pamoja na Walezi.

Sisi tunatarajia mwanafunzi:

  • Kuja muda unaofaa/bila kuchelewa.
  • Kuwasilisha taarifa zake kwa wakati.
  • Kuonyesha heshima kwa ajili ya mali ya shule, kwa Waalimu pamoja na wanafunzi wa pale shuleni.
  • Anashiriki kikamilifu wakati wa masomo. Kuwa na uwezo wa kuelezea jinsi mwanafunzi alivyokusidia kufikia jibu ni muhimu sana sawa na vile kupata jibu sahihi.
  • Kushiriki kikamilifu kwenye kazi ya kikundi, uchunguzi na majadiliano. Kwamba Mwanafunzi anafanya kazi pamoja kwa ushirikiano ili kufikia lengo linalotakiwa.
  • Kushiriki katika masomo ya vitendo kama kwa mfano maarifa ya nyumbani, michoro yaani picha za kuchorwa pamoja na muziki. Vipindi vya masomo haya ni muhimu kama zile za kinadharia/za nadharia/teoritiska.

Inatarajiwa kwamba Walezi watakuwa na mawasiliano na shule. Ushirikiano ulio mzuri kati ya shule na nyumbani kwa mwanafunzi inaleta manufaa kwa pande zote za wahusika. Kwa hivyo tutasikia kutoka kwako kwa yaliyo makubwa na madogo. Mshauri wa mwanafunzi/Mentor ndiye mnawasiliana naye wa kwanza.

Kazi yenye maadili

Maadili ya shule pamoja na kuwajibika kwake hutegemea msingi wa demokrasia na kwa hivyo hata uongozi wa Waalimu.

Elimu itafikisha na kuimarisha heshima ya haki za binadamu kwa kuzingatia ile misingi ya maadili ya kidemokrasia ambayo jamii ya Uswidi inategemea.

Thamani sawa ya Wanadamu wote, usawa kati ya Wanawake na Wanaume pamoja na mshikamano kati ya wanadamu ndiyo hasa maadili ambayo shule inapaswa kuunda na kufikisha. Mafundisho katika shule lazima yawe yasiyo ya madhehebu.

Shule inapaswa iweze kuunda na kufikisha yale maadili na haki zilizoonyeshwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa/FN:s Konvention kuhusu haki za Watoto (Mkataba wa haki za Watoto).

Habari kuhusu shule katika Manispaa ya Värmdö

Shule za Manispaa ya Värmdö

Katika Manispaa ya Värmdö kuna shule kumi za msingi za Manispaa na nne - zilizo huru.

Katika shule ya Hemmesta na shule ya Värmdö skärgårds kuna madarasa ya maandalizi ambapo wanafunzi wanaenda katika kikundi kidogo cha kufundisha ambayo ni sehemu ya siku ya shule. Wakati/muda uliobaki wanafunzi wanaenda kwenye darasa lao kubwa.

Mratibu

Wanafunzi wote wapya waliowasili pamoja na walezi wao kawaida wanakutana na Mratibu ambaye anafanya kazi kutoka Manispaa/Kommun ili kushiriki katika utafiti kuhusu lugha ya awali ya mwanafunzi pamoja na uzoefu wake wa shule. Matokeo ya utafiti huo huipatia shule uwezekano wa kufanya uwekaji yaani kupangwa vizuri na hata kuwapa Waalimu uwezekano wa kuyapanga mafundisho kwa kulingana na uwezo wa kiwango cha maarifa na uhitaji wa mwanafunzi.

Mshauri wa Mwanafunzi/Mwalimu wa darasa

Mshauri wa mwanafunzi/Mwalimu wa darasa ndiye mtu muhimu sana katika kuwasiliana na mwanafunzi na pia ni kiungo kati ya shule na nyumbani. Mshauri wa mwanafunzi/mwalimu wa darasa anafuata maendeleo ya maarifa ya mwanafunzi pamoja na maendeleo ya mwanafunzi katika jamiii yaani mwanafunzi katika jamii. Mshauri wa mwanafunzi/mwaliumu wa darasa anawajibika kwa hatua ambazo zinawekwa ikiwa mahitaji maalum yapo au yanatokea.

Darasa la maandalizi na Kiswidi kama lugha ya pili:

Darasa la maandalizi

Mwanafunzi ambaye anasoma katika darasa la maandalizi hupata mafunzo kwa sehemu katika kikundi kidogo cha kufundisha nje ya darasa ambalo huyo mwanafunzi amepangiwa yaani darasa lake. Kusudi hasa la FBK/darasa la maandilizi ni kwamba mwanafunzi lazima aweze kupata maarifa ya kutosha ya kiswidi ili kuweza kumudu mafunzo katika darasa kubwa. Mwanafunzi mmoja anafundishwa karibia miaka isiyopungua miwili katika darasa la maandilizi/FBK.

Kiswidi kama Lugha ya Pili:

Wanafunzi ambao wana ujuzi wa kutosha wa lugha kuweza kufanikisha ufundishaji katika darasa kubwa, hukaribishwa mafunzo ya kiswidi kama lugha ya pili ambayo hutolewa ili kuimarisha na kukuza lugha ya kiswidi. Mtaala wa kiswidi kama lugha ya pili ni sawa na somo la kiswidi, lakini mwanafunzi anapimwa kwa kuzingatia lugha nyingine ya Mama yaani Lugha-zazi.

Mawasiliano kati ya nyumbani na Shule:

Shule zilizopo katika Manispaa/Kommun huwa zinawasiliana na wanafunzi pamoja na walezi kwa kupitia chombo cha msingi wa waruti, inayoitwa jukwaa la shule/skolplattform; Schoolsoft (wanawasiliana walezi/wanafunzi/waalimu). Huko munatoa ripoti ikiwa mwanafunzi anaumwa hivyo atabaki nyumbani, wasiliana na Mshauri wa mwanafunzi/Mwalimu wa darasa na kufuata ukuaji wa maarifa yaani maendeleo ya mtoto wako kwa njia ya hakiki, thathimini na alama/marksi. Mshauri wa mwanafunzi/Mwalimu wa darasa huwa ndiye pia anayeweka nyakati kwa ajili ya mazungumzo ya maendeleo ya mwanafunzi katika schoolsoft ambako ndiko mnakojiandikisha ule muda unaowafaa kwa mazungumzo husika.

Wakati wa mazungumzo haya kati ya Watoto, Walezi na Waalimu, kwa njia hiyo kwa sehemu unashiriki kufahamu jinsi ambavyo mambo yanavyokwenda shuleni, katika masomo tafauti pamoja na kama nyie Walezi mnakuwa na maswali yoyote.

Kwenye Schoolsoft pia ndiko ambako mnapata habari taarifa/infomesheni kuhusu mikutano ya Wazazi. Mikutano hiyo huwa inahusu taarifa za jumla kutoka kwa mwalimu mkuu kuja kwenu ninyi walezi.

Maelezo ya namna ya kuingia katika mtandao mnayapata kutoka kwenye ofisi ya mapokezi ya shule/expedition.

Shughuli baada ya Shule

Shughuli mbalimbali baada ya masaa ya shule huwa zinachangia kwenye maendeleo ya ukuaji wa lugha lakini pia katika mawasiliano ya kijamii na ujumuishaji. Kwa maana hiyo inaweza kuwa jambo zuri lenye manufaa endapo mwanafunzi atabakia shuleni pamoja na marafiki zake baada ya yale masaa ya kawaida ya shule. Kwa wanafunzi wadogo zaidi ambao wanaenda darasa la shule ya mapema/chekechea hadi darasa la tatu (3), hao hupewa nafasi za wakati wa kupumzika kwenye nyumba ya burudani ambapo huko wako hucheza-cheza na kwa ajili ya wanafunzi wakubwa kidogo wanaosoma madarasa ya 4, 5, na 6 nao pia hupewa nafasi za wakati wa kupumzika kwenye nyumba ya burudani ambapo shughuli wazifanyazo hapo hufanana na zile za wanafunzi wengine(wadogo) isipokuwa hapo shughuli kama hiz hufanyika kwenye sehemu ambayo huitwa Klubben.

Katika umri mkubwa inaweza kuwa vizuri kushiriki katika michezo, kwa mfano mazoezi ya kucheza mpira/soka/kabumbu. Kwa kufanya mazoezi ya mwili kama hayo pia ni kukuza afya pamoja na kwamba inaleta faida nyingine nyingi.

Muda wa kuwa huru/Ruhusa

Wanafunzi wako huru kutoka shuleni wakati wa likizo (ruhusa). Uhitaji wa likizo/ruhusa kwa wakati mwingine kwa jumla, inapaswa uombe kutoka kwa Mshauri wa mwanafunzi au Mwalimu mkuu. Maombi ya maandishi yanawasilishwa kwa Mshauri wa mwanafunzi. Wakati wa likizo ya shule, nyumba ya burudani yaani kucheza-cheza na kupumzika inakuwa wazi kwa wanafunzi wa umri mdogo, hata hivyo. Wewe kama Mlezi unahitajika kuomba hili kwa wakati ulio mzuri yaani mapema.

Timu ya afya ya wanafunzi

Katika kila shule ya Manispaa kwenye Manispaa ya Värmdö/Värmdö kommun kunakuwa na timu moja ya afya ya wanafunzi yenye kuwa na Nesi/Muuguzi wa shule. Mshauri/kurator, Mwalimu maalum/specialpedagog, Waalimu maalum/speciallärare. Mshauri wa masomo ya taaluma pamoja na Mwalimu mkuu msaidizi. Daktari wa shule na Saikolojia wa shule wanapatikana kazini lakini hawajapangiwa (ofisi)/hawajawekewa katika shule maalum.

Wajibu wa timu hiyo ni kuongezea uwezo wa ufundishaji (ualimu) kuhusu maendeleo ya wanafunzi na namna ya wanafunzi hao yawabidi kujifunza yaani ujifunzaji. Pamoja na waalimu na wafanyakazi wengine wa shule, timu inafanya kazi kuchangia hali nzuri ya kujifunza iwezekanavyo kwa wanafunzi.

Fomu za kujaza na kuwasilisha:

SOS-Fomu/SOS-blankett - Ni fomu yenye taarifa kuhusu mwanafunzi pamoja na anwani na namba ya simu ya Mlezi. Katika hiyo fomu pia hujibiwa maswali kuhusu dawa/ujuzi wa kuogelea/kupigwa picha. Fomu hiyo inapaswa kuwasilishwa kwa Mshauri wa mwanafunzi/Mentor.

Chakula maalum/specialkost - Ikiwa mwanafunzi kutokana na sababu ya mzio/kudhurika/allegi au sababu ya dhini anakuwa na uhitaji wa chakula fulani ambacho ni maalum. Fomu hiyo inapaswa kuwasilishwa kwa Mshauri wa mwanafunzi.

Nyumba ya burudani/Fritids/Klubben - Wanafunzi wanaoenda katika darasa la shule la mapema na kwenye madarasa ya 1-6 wanaweza kuomba nafasi katika nyumba ya burudani (kucheza-cheza) pamoja na shughuli zinazofanana na hizo za kwenye Klubben. Fomu hiyo inapaswa kuwasilishwa kwa Mshauri wa mwanafunzi.

Kompyuta/Dator - Kutoka darasa la 4, wanafunzi wanaweza kuazima kompyuta kama zana yaani chombo cha kujifunzia. Mlezi na mwanafunzi kwa pamoja lazima wasome utaratibu yaani kanuni/masharti ambayo yahusika katika muda wa kuazimishwa pia kuweka sahihi kwenye mkataba huo. Mlezi ndiye ambaye anawajibika. Fomu hiyo inapaswa kuwasilishwa kwa Mshauri wa mwanafunzi.

Kufundisha Lugha-zazi/Modersmålsundervisning - Inaruhusiwa katika lugha kadhaa na inapendekezwa sana. Utafiti unaonyesha kwamba mafunzo ya Lugha-zazi inakuwa bayana yaani wazi, ina athari nzuri zilizo wazi juu ya ukuaji wa maarifa ya mwanafunzi shuleni katika masomo yote.

Kufundisha kunatawaliwa na mtaala na mtaala wa somo yaani kufuata mpango wa masomo kwa jumla kiasi kwamba hatimaye mwanafunzi anaweza kupata alama katika somo hilo.

Maombi yanatumwa kwa: Farstavikens Skola/Modersmål Bergsgatan

134 41 Gustavsberg.

Kadi ya Basi/Busskort - Mlezi anaomba mwenyewe kuhusu kadi ya Basi katika Manispaa ya Värmdö/Värmdö kommun. Mwanafunzi ambaye anaishi ndani ya kilomita 4/4km kutoka shuleni, walio wengi hawapewi kadi za Basi. Kama mtu anapewa huyo anapaswa kuichukua hiyo kadi ya Basi katika ofisi ya mapokezi ya shule/expedition.